Mwanamitindo
Hamisa Mobetto amejibu iwapo yupo tayari kufunga ndoa Diamond Platnumz
mara baada ya muimbaji huyo kuweka wazi atafanya hivyo mwaka huu.
Akizungumza
katika uzinduzi wa Filamu ya Mama kutoka kwa Aunt Ezekiel, Hamisa
alipoulizwa iwapo yupo tayari kuolewa na Diamond alijibu kwa sasa huwezi
kuzungumzia hilo.
“Siwezi kujibu hilo swali,” aliongea Hamisa kwa kifupi.
Katika hatua nyingine Hamisa alidai kuwa yeye sio single mother kwani wazazi wenzie wanamsaidia katika malezi ya watoto.
“You
can’t call your self Single Mother kama unasaidiwa kulea mtoto na baba
watoto wako, so facts is mababa watoto wangu wote wananisaidia kulea
watoto vizuri, kwa hiyo siwezi nikasema single mother sababu nasaidiwa
kulea watoto,” alisema Hamissa.
Hamisa ni mama wa watoto wawili ambao wa kwanza alizaa na Majay na wapili alizaa na Diamod Platnumz.
0 comments:
Post a Comment