Mamlaka
ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imetoa tahadhari ya kunyesha mvua kubwa
kwa siku tano kuanzia jana, ambazo zinaweza kuleta mafuriko katika
maeneo ya mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara na Visiwa
vya Unguja na Pemba.
Katika taarifa ya TMA iliyotolewa jana Mei 13, mvua hizo zilizoanza kunyesha zitaendelea mpaka Mei 17 mwaka huu.
TMA
imesema athari zinazinaweza kutokea ikiwemo mafuriko ambayo yanaweza
kusababisha kuvurugika kwa usafiri, barabara kubwa kutopitika na maisha
ya watu kuwa hatarini kutokana na maji kujaa au kupita kwa kasi.
Pia
imetoa wito kwa wakazi wa maeneo hayo kuchukua tahadhari stahiki na
kuendelea kufuatilia taarifa pamoja na tahadhari zitakazotolewa.
0 comments:
Post a Comment