Mbunge
wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye amemkaribisha uraini Mbunge wa Mbeya
Mjini,Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ baada ya kutoka gereza la Ruanda alipokuwa
akitumikia kifungo chake .
Nape amesema kuwa anakumbuka Mbunge huyo ambaye pia ni msanii aliwahi kuimba juu yake wakat alipoanza siasa.
“Karibu
tena Uraini brother!{nakumbuka uliwahi kuimba juu yangu wakati huo
nilipoanza siasa},” ameandika Nape kupitia ukurasa wake Twitter.
Sugu
na katibu wa Chadema kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga walitiwa hatiani
na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano jela February 26, 2018 kwa kutoa
lugha ya fedhea dhidi ya Rais John Magufuli kwenye mkutano wa hadhara
walioufanya Desember 30, 2017 katika uwanja wa shule ya msingi Mwenge,
Mbeya
0 comments:
Post a Comment