Hospitali
ya Taifa Muhimbili (MNH), imekiri kuharibika kwa moja ya mashine zake
za CT-Scan hali inayolazimu wagonjwa kupimwa kwa kutumia mashine moja
ambayo ni mpya.
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja wa Muhimbili,
Aminiel Aligaesha alithibitisha kuharibika kwa mashine hiyo jana.
“Ni
kweli mashine yetu moja ya CT Scan, ile ambayo ilikuwa inatumika kwa
muda mrefu hapa hospitalini imeharibika si chini ya miezi mitatu sasa,”
alisema.
Eligaesha
alisema hivi sasa madaktari wanalazimika kuwafanyia uchunguzi wagonjwa
katika mashine mpya iliyonunuliwa na Serikali miaka miwili iliyopita.
“Hii
mpya haina tatizo lolote, MOI (Taasisi ya Mifupa Muhimbili),
wanatarajia kufunga CT-Scan mpya, tutakuwa tunashirikiana nao
kuwachunguza wagonjwa,” alisema.
Alipoulizwa
iwapo pamoja na ushirikiano huo, Muhimbili itanunua mashine mpya
nyingine ya CT-Scan, alisema hawana mpango huo kwa sasa.
“Mashine
hizi ni gharama kubwa mno, ni kati ya Sh. bilioni mbili hadi tatu hivi,
kwa kuwa MOI watafunga, tutaendelea kushirikiana nao pamoja na yetu
kusaidia wagonjwa,” alisema.
0 comments:
Post a Comment