Rais
wa Marekani, Donald Trump ametilia shaka kuhusu kufanyika kwa mkutano
na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un mwezi june mwaka huu huko
Singapore.
Ameyasema
hayo mara baada ya Korea Kaskazini kutishia kujiondoa katika mkutano
huo endapo Marekani itaendelea kusimamia msimamo wake wa kuiwekea
vikwazo nchi hiyo.
Aidha,
Rais Trump hakuweka wazi ni masharti gani ambayo yamewekwa kwa ajili ya
mkutano huo,na alipoulizwa na waandishi wa habari juu ya masharti
aliyoiwekea Korea Kaskazini amesema kuwa suala la kuachana na silaha za
nyuklia ni lazima litekekelezwe na Korea Kaskazini.
Mkutano
kati ya rais Trump na Kim Jon-un uanatarajiwa kufanyikwa June 12 nchini
Singapore ukitanguliwa na mkutano wa marais wa Korea hizo mbili
uliofanyika mwezi April.
Hata hivyo, ameongeza kuwa mwelekeo wa Kim Jong-un umebadilika baada ya ziara yake ya pili mwezi huu nchini China.
0 comments:
Post a Comment