Serikali
ya Zanzibar imeagiza zaidi ya waalimu 300 wa masomo ya Sayansi kutoka
nchini Nigeria ambao tayari wameanza kuwasili visiwani humo.
Kwa
mujibu wa serikali ya Zanzibar, waalimu hao wanaoingia kwa awamu, na
wanatarajiwa kuziba pengo la uhitaji wa zaidi ya waalimu 300 wa masomo
hayo.
Naibu
waziri wa Elimu Zanzibar Mmanga Mjengo amesema ujio huo utasaidia
kuamsha pia morali ya waalimu wengine wa masomo ya sayansi visiwani
humo.
Ameongeza
pia wameamua kwenda Nchini Nigeria kwa sababu kuna wingi wa waalimu na
wenye ubora na haikuwa rahisi kuchukua kutoka nchi za karibu kwa sababu
na wao pia wana tatizo la uhaba wa waalimu.
''Mchakato
wa upatikanaji wa waalimu hawa hufanywa kwa kutegemea uwezo wao katika
ufundishaji na pia ubora wa kazi zao.'' alisema waziri Mjengo.
Serikali
ya Zanzibar imesisitiza kuwa sio mara ya kwanza kwa ujio kama huu kwani
katika miaka ya nyuma waalimu hawa wamekua wakija kwa kujitolea.
Ujio
wa waalimu hawa ambao watakuwepo kwa kipindi cha miaka miwili unatajwa
kupunguza uhitaji wa zaidi ya waalimu 300 visiwani humo.
0 comments:
Post a Comment