Mke
wa Prodyuza maarufu na mkongwe kwenye mziki wa Bongo fleva P Funk
majani, Samira ameibuka na kudai atapambana na Kajala na kamwe
hatamuachia nyumba.
Kwa
Miezi kadhaa Kumekuwa na tetesi kuwa PFunk na Ex wake ambaye pia ni
mama watoto wake aliyezaa naye mtoto mmoja Kajala wamerudiana kitu
kinachomuweka Pabaya mke wa Pfunk ambaye hivi sasa ni mjamzito.
Samira
ambaye wiki iliyopita ilisemekana alikuwa tayari kumuacha Pfunk na
kurudi kwa wazazi wake Arusha, inadaiwa ameamua kupambana na Kajala na
kukataa kumuacha Kajala amchukue mumewe.
Kwenye
mahojiano na GPL, Samira ameongea kwa uchungu huku akidai kila siku
huwa anaumizwa pale anapokutana na kashfa kumuhusu mume wake na Kajala
lakini ameamua kubaaki kupambana.
"Yaani
mateso ninayokutana nayo kwenye ndoa yangu ni Mungu pekee ndio anajua
tena kwenye hali hii ya ujauzito niliyo nayo, awali nilipanga niondoke
nimuachie nyumba lakini nimeona nikomae hadi kieleweke“.
Mara
nyingi Kajala alipokuwa akiulizwa kuhusiana na kuingilia ndoa hii ya
mzazi mwenzie amekuwa akikana na kusema kuwa kuwa P Funk ni baba wa
mtoto wake na si vinginevyo ingawa video mbalimbali zinavuja zikiashiria
ni wapenzi.
0 comments:
Post a Comment