Mwanamuziki
wa Bongo fleva Nandy amefunguka na kudai alikuwa tayari kuacha muziki
baada ya ile video yake chafu kuvuja Kwenye mitandao ya kijamii.
Wiki
chache zilizopita Nandy aliwaacha watu midomo wazi baada ya video yake
iliyomuonyesha akiwa kitandani na aliyekuwa mpenzi wake Billnas
kuvujishwa Kwenye mitandao ya kijamii.
Nandy amekiri kutaka kuacha muziki Kwenye mahojiano na Kipindi cha leo Tena cha Clouds Fm ambapo amesema;
"Nilihisi
kukata tamaa na kuachana na muziki kabisa maana sikuona maana ya
maisha. Lakini nilipofika BASATA walinipa ushauri na kunihoji kama kweli
nilivujisha picha zile kwa ajili ya Kiki, ... binafsi sikuwa na picha mbaya nyuma katika maisha yangu
"
Hali yangu ilikuwa mbaya sana nilipoona ile video sikuamini kabisa
macho yangu. Nilizidiwa na Pumu nikakimbizwa hospitali kifupi nilipata
Brain Attack niliwaza kuhusu familia yangu nItamtazamaje mama na baba
yangu?”.
Nandy jana aliachia wimbo wake mpya ulioandikwa na msanii mwenzake Aslay unaoitwa Ninogeshe.
0 comments:
Post a Comment