Sophia
Salehe, mkazi wa Kata ya Namiongo, Newala mkoani Mtwara, anashikiliwa
na Jeshi la Polisi mkoani humo, kwa tuhuma za kumuua mume wake kwa
kumchoma kwa kisu.
Mauaji
hayo yalitokana na ugomvi baina ya mtuhumiwa ambaye inadaiwa kuwa
alikataa wito wa mumewe kupika chakula baada ya kutokushiba.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Lucas Mkondya, amesema tukio hilo lilitokea juzi mkoani humo.
Kwa mujibu wa Mkondya, mwanamume huyo alikufa papo hapo baada ya kuchomwa kisu na mke wake.
Alisema siku ya tukio majira ya saa 1:30 usiku, mwanamke huyo alimwandalia mume wake chakula na kumpatia.
“Kile
chakula kilikuwa kidogo, mume wake, Ahmed Salim, alimtaka arudi jikoni
kwa ajili ya kupika tena chakula kwa kuwa hakikumtosha. Hapo ndipo
palitokea ugomvi wakalumbana na wakaendelea kugombana na mkewe akachukua
kisu na kumchoma kifuani,” alisema Kamanda Mkondya.
Kamanda Mkondya alisema Salim alifariki dunia papo hapo baada ya kutokwa na damu nyingi kwenye jeraha.
Aidha,
alisema katika tukio hilo wanamshikilia na mwanaume mmoja ambaye
hakutaka jina lake liandikwe kutokana na uchunguzi unaoendelea.
Alisema
wanamshikilia kijana huyo kwa kuwa katika tukio hilo alikuwapo, hivyo
watakapopata maelezo yatakayojiridhisha kutohusika ataachiwa.
“Bado
huyu kijana tunamhoji ni kwa nini hakutoa msaada wa kuamua ugomvi huo.
Hapa tunataka kujua na yeye amehusika au la na kwa huyu mwanamke
taratibu zikikamilika atafikishwa mahakamani,” alisema.
Aidha,
Kamanda alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya
Wilaya ya Newala kwa ajili ya kusubiri taratibu za mazishi.
0 comments:
Post a Comment