Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema
kuwa amesikitishwa na vitendo vya Mabalozi kushindwa kutekeleza maagizo
yake aliyowapa ya kumpa taarifa juu ya utendaji kazi wao na manufaa
ambayo Tanzania imeyapata kwa uwepo wa kila Balozi katika nchi
aliyopangiwa kila robo mwaka.
Ameyasema
hayo Ikulu Jijini Dar es salaam mara baada ya kumaliza kumuapisha,
Alphayo Kidata kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada na Msalika Robert
Makungu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa T abora.
Amewataka viongozi hao kwenda kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa na kwa manufaa ya Taifa na sio kufanya mambo ndivyo sivyo.
“Balozi
ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania katika nchi fulani, nchi imenufaikaje
na uwepo wake kwenye nchi ile?. Kuteuliwa sawa lakini sio lazima ukae
katika ubalozi huo kwa kipindi chote ulichopangiwa, ukishindwa kuleta
manufaa unarudishwa na huko anapangiwa mtu mwingine atakayeleta manufaa
kwa nchi,”amesema Rais Dkt. Magufuli
Hata
hivyo,Rais Dkt. Magufuli ameipongeza Wizara ya Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa kufanya kazi nzuri katika sekta ya
Elimu na Afya
0 comments:
Post a Comment