Muimbaji
mwenye sauti aina yake kutoka Bongo, Ray C amesema ukali wa Rais
Magufuli umepelekea wasanii waliokuwa na tabia ya kupiga picha za utupu
kuacha.
Ray C akiwa nchini Kenya amesema tabia hiyo kipindi cha nyuma ilishamiri ila kwa sasa inaenda ikipungua.
“I
don’t know lakini inakuwa too much inaenda inakuwa too much ndio maana
Rais Magufuli kakataza, siunajua Baba yetu mkali kidogo. It was too much
ilikuwa inaanza kwenda mbali, unajua watoto wanaangalia,” Ray C
ameiambia Citizen TV.
Alipoulizwa kwanini yeye hafanyi hivyo alijibu; “Sinitapelekwa jela na Rais Magufuli, yeah!, is not allowed,”.
Mapema
January mwaka huu Serikali ilimuita msanii Gigy Money na Mwanamitindo
Sanchoka kwa mahojiano maalumu kuhusu kazi zao ambazo zilionekana zipo
kinyume na maadili hususani kwenye mavazi wanayovaa.
0 comments:
Post a Comment