Waziri Mkuu wa zamani Najib Razak na mkewe Rosmah Mansor wamezuiwa kuondoka nchini, Idara ya Uhamiaji imesema Jumamosi.
Taarifa
ya Idara ya Uhamiaji ilitolewa muda mfupi baada ya kiongozi huyo wa
zamani mwenye kashfa ya ufisadi kuandika katika Facebook kwamba yeye na
familia yake wanatarajiwa kwenda ughaibuni kwa mapumziko kuanzia
Jumamosi na watarejea wiki ijayo.
Katika akaunti ya Twitter Najib amesema ataheshimu amri ya kuzuiwa iliyotolewa na serikali kumtaka asiondoke nchini.
"Nimetaarifiwa
kwamba Idara ya Uhamiaji imenizuia mimi na familia yangu kusafiri nje
ya nchi. Naheshimu amri na nitabaki nchini na familia yangu,” ameandika
Najib.
Waziri
mkuu huyo aliyeondolewa kupitia sanduku la kura sasa anachunguzwa na
Serikali juu ya tuhuma za ufisadi wa fedha za uwekezaji ambazo maofisa
wanadaiwa kuiba zaidi ya dola za Marekani 4.5bilioni.
Inadaiwa kiasi kingine cha fedha kiliishia kwenye akaunti binafsi ya Najib katika benki.
Najib
amekanusha kufanya kosa lolote na anasema fedha hizo zilitolewa na
familia ya kifalme ya Saudi Arabia na kwamba alikwisharejesha.
0 comments:
Post a Comment