Na Bashiri Salum, Dodoma
Serikali
imeagiza sukari kiasi cha tani 70,354.35 kutoka nchi za nje lengo
likiwa ni kujipanga ili kuhakikisha kuwa hapatokei upungufu wa bidhaa
hiyo hapa nchini.
Akizungumza
na vyombo vya habari hivi karibuni waziri wa kilimo Mhe. Dkt. Charles
Tizeba amesema kuwa tani 60,539.35 ya sukari itaanza kuingia hapa nchini
katikati ya mwezi Mei 2018 ambapo kiasi kilichobaki cha tani 9,815
kitaingia mwezi June mwaka 2018.
Aidha
Dkt. Tizeba amefafanua kwamba hakutarajiwi kuwa na upungufu wa sukari
hapa nchini kwa sababu hadi kufikia tarehe 10 mei 2018 katika maghala
ya wazalishaji na wafanyabiashara kulikuwa na tani 78,147.67 za sukari
na kiasi kingine tani 25,441.25 kipo Bandarini .
Kwa
kiasi cha sukari ambacho tayari kipo hapa nchini kikijumlishwa na kiasi
ambacho kitaingia hivi karibuni kutoka nje ya nchi ni dhahiri kwamba
nchi haiwezi kupata upungufu wa bidhaa hiyo, alisema Mhe.Waziri.
Awali
Dkt.Tizeba alisema kwamba mahitaji ya sukari nchi nzima ni tani
630,000 ambapo kati ya hizo, tani 145,000 ni kwa ajili ya matumizi ya
viwandani na tani 485,000 ni kwajili ya matumizi ya kawaida.
Hata
hivyo mapitio yanaonesha kwamba msimu wa mwaka 2017/18 viwanda vya
ndani vilizalisha tani 306,226 za sukari kwa matumizi ya kawaida
ambapo mwisho wa msimu huu uzalishaji umefikia tani 307,481.76
aliongezea Dkt. Tizeba.
Akimalizia
taarifa yake Mhe. Tizeba amebainisha kuwa kwa kiasi ambacho sukari
imeagizwa kutoka nje Pamoja na viwanda vya ndani inadhihirisha kwamba
hakutakuwa na upungufu wa aina yeyote ya sukari hapa nchini na
ikizingatiwa kuwa viwanda vitaanza uzalishaji mwingine mwezi mei ambapo
ukarabati (services ) itakuwa imekamilika .
0 comments:
Post a Comment