Ngombe
12 wanaosadikiwa kufa jana wamekutwa wakichinjwa ndani ya lori eneo la
mtaa wa Wazo kwa ajili ya kusambazwa kwenye mabucha ya ngo’mbe.
Mmoja wa mashuhuda Issa Ibrahim amesema wakati anaelekea msikitini jana saa 10 alfajiri aliliona gari aina ya lori limesimama pembezoni mwa barabara na alipolisogelea aliwaona watu wakiwachuna ng’ombe waliokufa.
Amesema
aliwahoji na kuwakataza wasiendelee kuwachuna ngombe hao kwa kuwa dini
hairuhusu kula vibudu lakini watu hao walikaidi na kuendelea kazi yao.
“Wale
watu walikuwa wengi kila mmoja alikuwa na kisu chake huku wakichuna
ngombe hao, kwa kuhofia usalama wangu nilipiga simu msikitini ndipo
walikuja eneo hili ili tuungane tuweze kuwakamata lakini wote walikimbia
na kuacha nyama zao kwenye gari,” amesema Ibrahim.
Katibu
wa Kamati ya Afya na Mazingira mtaa huo, Ally Kitokos amesema matukio
ya kuchinjwa ng’ombe waliokufa hujitokeza mara kwa mara na ndiyo maana
hivi karibuni mmiliki wa machinjio ya Wazo alimfukuza kazi mchinjaji
mkuu baada ya kupingana na kitendo cha kuchinja ngombe waliokufa.
“Leo
hii tunaona ng’ombe 12 wamekufa kibudu na wanaendelea kuwachuna kwa
ajili ya kupelekwa kwenye mabucha, wakati mchinjaji mkuu wa mwanzo
alifukuzwa kwa kosa hilo,” amesema.
0 comments:
Post a Comment