Serikali
imetangaza nafasi za kazi zaidi ya 6,180 katika sekta ya afya nchini na
kuwataka wananchi wenye sifa stahiki kuomba nafasi hizo ili kuweza
kutatua changamoto ya upungufu wa watumishi katika vituo vya Afya,
Zahanati na Hospitali za Wilaya.
Akiongea
na waandishi wa habari jana Mei 10, 2018 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo alisema
watumishi hao wataajiliwa kabla ya mwaka kuisha na kuongeza kwamba lengo
la serikali ni kuboresha sekta ya afya nchini.
“Naomba
niwataarifu kwamba serikali ofisi ya TAMISEMI imepata kibari cha
kuajiri watumishi wapya 6,180, watumishi hawa tunatarajia kuwa ajiri
hivi karibuni kabla ya mwaka huu kuisha kwa hiyo napenda kuutangazia
umma kuwa dirisha la ajira lipo wazi, kwa watu wote wenye sifa
kuhakikisha wanaomba nafasi hizo lengo kubwa ni kupata watumishi
kwaajili ya vituo vya afya vipya tunavyovijenga” alisema Jafo.
Waziri
Jafo amliongeza kuwa watumishi waliokua wanajitolea watapewa kipaumbele
zaidi; “kuna vijana wengine wamemaliza taaluma yao na hawataki ipotee
wameamua kuomba nafasi mbalimabi kwa ajili ya kujipa uzoefu kwahiyo watu
hao watakua kipaumbele chetu cha kwanza katika kuwaingiza katika ajira”
Waziri
wa Tamisemi amesema serikali inakamilisha ujenzi wa vituo vya afya 208
ambavyo vitagharimu shilingi bilioni 156 katika ujenzi wa miundombinu na
vifaa tiba, pia serikali inajenga hospitali kubwa za wilaya takribani
68 na zitagharimu shilingi bilioni 105.
Watakaoajiriwa
ni wenye sifa zifuatazo, Awe raia wa Tanzania, kuambatanisha nakala ya
cheti cha kuzaliwa, kidato cha nne na sita, cheti cha taaluma na asiwe
muajiliwa wa serikali au shirika la dini ambapo mshahara wake unalipwa
na serikali, umri usizidi miaka 45 na utayali wa kufanyakazi mahali
popote nchini
0 comments:
Post a Comment