Mbunge
wa Mbeya Mjini (CHADEMA) Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu amesema
anajiona shujaa baada ya kufanikiwa kutoka gerezani na kusema kuwa
amepata hisia walizopitia viongozi waliofungwa kisiasa duniani.
Sugu
amesema hayo jana Mei 10, 2018, wakati akiongea na vyombo vya habari
nyumbani kwake Mjini Mbeya muda mfupi baada ya kuachiwa huru, na kusema
kuwa yeye alifungwa kisiasa na ndiyo maana anajiona shujaa kwasabau
ameingia katika kundi moja la vingozi wa zamani kama Hayati Nelson
Mandela wa Afrika Kusini.
"Najisikia
shujaa kuingia kundi la wafungwa wa kisiasa duniani, Mandela, Obasanjo,
ingawa ni kwa muda mfupi lakini zile hisia alichokua anajisikia Mandela
wakati yupo ndani, katikati ya usiku haupo na familia hizo hisia
ninazo" amesema Sugu.
Sugu
alitumia muda huo kuwapa pole wakazi wa jimbo la Mbeya mjini kwa sababu
muda mrefu walimkosa Mbunge huyo na kudai kuwa yeye alifungwa kimwili
ila wakazi wa jimbo hilo walifungwa mioyo.
Mbunge
Sugu na Katibu wa Chadema kanda ya nyanda za juu kusini Emmanuel
Masonga, waliachiwa huru jana Mei 10, 2018 baada ya kuhudumu katika
Gereza la Ruanda mkoani mbeya kwa siku 73 ambapo taarifa ya Gereza hilo
imedai wawili hao walitolewa kwa msamaha wa Rais John Magufuli alioutoa
katika sherehe za siku ya muungano April 26, 2018.
February
26, 2018 Mahakama ya Hakimu mkazi Mbeya iliwatia hatiani Sugu na
Masonga na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano jela kwa kosa la kutumia
lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli katika mkutano wa hadhara
uliofanyika Disemba 30, 2017
0 comments:
Post a Comment