WAZIRI
Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali ipo tayari kwa maandaalizi ya
fainali za michuano ya Afrika ya vijana wenye umri chini ya miaka 17
mwaka 2019.
Mashindano ya mpira wa miguu kwa Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 AFCON yanayotarajiwa kufanyika mwakani nchini Tanzania.
Ameyasema
hayo jana (Alhamisi, Mei 10, 2018) wakati akijibu swali la Mbungewa
Sumve Bw. Richard Ndassa katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa
Waziri Mkuu, Bungeni Jijini Dodoma.
Katika
swali lake Bw. Ndassa alitaka kujua Serikali imejipangaje kufanikisha
mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 baada ya Shirikisho la
Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) kuipa Tanzania uenyeji wa fainali
hizo.
“Maandalizi
ya fainali hizo yanaendelea vizuri, hivyo nawaomba Watanzania wenzangu
tuendelee kuziunga mkono timu zote zinazofikia mashindano ya kimataifa
ili ziweze kufanya vizuri”.
Waziri
Mkuu alisisitiza kwamba “ni jukumu letu kuziandaa timu zote ambazo
zinashiriki mashindano ya kimataifa ili ziweze kuibuka na ushindi.”
Hata
hivyo alisema analishukuru Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutokana
na maandalizi yanaendelea ikiwa ni pamoja na kuipeleka timu nchini
Sweden.
Pia
Waziri Mkuu alisema Wizara ya Maliasili na Utalii itatumia mashindano
hayo kwa kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini.“Tutawapeleka
Kilwa wakaone majengo ya zamani yaliyokaliwa na Waarabu na maeneo
mengine.”
Waziri
Mkuu amewasihi Watanzania kutumia fursa ya mashindano hayo
yanayotarajia kufanyika nchini kwa kufanya shughuli mbalimbali
zitakazowaongezea kipato.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
0 comments:
Post a Comment