Serikali
imesema ipo haja ya kuridhia mkataba wa kupambana na silaha za baolojia
na sumu ili kuweza kutoa fursa kwa wataalamu mbalimbali nchini katika
kuwajengea uwezo wa kukabiliana na athari za mashambulizi ya silaha za
sumu na kibaoloji.
Kauli
hiyo imetolewa leo Mei 11, 2018 na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga
Taifa (JKT) Dkt. Hussein Mwinyi Bungeni Jijini Dodoma kwenye kikao cha
28 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
wakati akijibu la akijibu swali la Mbunge wa viti maalum Jasson Rweikiza
aliyetaka kujua ni kwa nini Tanzania haijajiunga na mkataba wa
kupambana na silaha za sumu (Biological Weapons Convention).
"Tanzania
ilisaini mkataba wa kupambana na silaha za baolojia na sumu tarehe 1
Agosti, 1972 lakini mpaka sasa haijaridhia mkataba huo, kutoridhiwa kwa
mkataba huo kulitokana na kutoonekana athari zake za moja kwa moja kwa
wakati huo ambapo matumizi salama ya mkataba ikiwemo utafiti wa magonjwa
ya binadamu, wanyama na mimea yameendelea kufanyika nje ya mkataba huo.
Changamoto zinazotokana na matishio mbalimbali ikiwemo ugaidi,
zimesababisha hitaji la kuridhiwa kwa mkataba huo na kutekelezwa kwa
vitendo baada ya kutungiwa sheria", amesema Dkt. Mwinyi.
Pamoja na hayo, Dkt. Mwinyi ameendelea kwa kusema
"Serikali
inafahamu madhara yaliyopo hivi sasa ya kutoridhiwa kwa mkataba huo
ikiwemo Tanzania kuwa katika kundi dogo la nchi ambazo hazijaridhia
mkataba huo kama vile Haiti, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Misri, Somalia
na Syria ambapo Tanzania kuwepo katika kundi hilo hakutoi taswira nzuri
kwa jamii ya Kimataifa kwani kati ya nchi hizo nyingi zina migogoro ya
muda mrefu ya ndani....
"Kuwanyima
fursa wataalamu wetu kupata mafunzo mbalimbali yanayotolewa katika
kujenga uwezo wa kukabiliana na athari za mashambulizi ya silaha za sumu
na kibaolojia na pia kunanyima fursa kwa wataalamu na viongozi wa
kitanzania kushiriki kwenye uongozi wa taasisi mbalimbali za kimataifa
zinazosimamia sheria za silaha za kibaolojia na sumu".
Kwa
upande mwingine, Dkt. Mwinyi amesema teyari waraka umeshaandaliwa na
muda si mwingi utapelekwa Bungeni kwa ajili ya kuridhiwa ambapo ameahidi
mpaka kufikia Septemba 2018 utakuwa umeshawasilishwa.
0 comments:
Post a Comment