Shirikisho
la soka nchini TFF leo Mei 16, limethibitisha kuwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekubali ombi la kuwa
mgeni rasmi na kukabidhi vikombe vya ubingwa wa Serengeti Boys na Simba.
Mtendaji
mkuu wa TFF Wilfred Kidao amesema wamethibitishiwa na Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kuwa Rais Magufuli
amekubali kuwa mgeni rasmi kwenye mchezo wa Simba SC dhidi ya Kagera
Sugar jumamosi hii.
''Rais
Magufuli amekubali ombi la TFF kuwakabidhi vijana wa Serengeti Boys
Kombe la CECAFA waliloshinda hivi karibuni nchini Burundi, tukio ambalo
litaambatana pia na kuikabidhi Simba SC kombe la ubingwa wa VPL msimu
huu'', amesema.
Serengeti
Boys wameibuka mabingwa wa soka katika ukanda wa Africa Mashariki na
Kati baada ya kutwaa ubingwa huo kwa kuwafunga vijana wa Somalia kwa
mabao 2-0 kwenye mchezo wa fainali.
Simba
imetwaa ubingwa wa Ligi kuu soka Tanzania Bara msimu wa 2017/18 baada
ya kufikisha alama 68 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kati ya 16
za ligi kuu msimu huu.
0 comments:
Post a Comment