Mvua kubwa yatarajiwa kunyesha katika mikoa ya Dar es salaam, Tanga, Pwani na Visiwa vya Unguja na Pemba.
Utabiri
huo umetolewa na Mamlaka ya Utabiri wa Hali ya Hewa Nchini (TMA), ambao
umeeleza kuwa kiwango hicho cha mvua kilitarajiwa kuanza jana usiku.
Kwa
mujibu wa utabiri huo kiwango cha mvua hiyo kitaendelea kwa siku tano
hasa wanaoishi mabondeni, wametakiwa kuchukua tahadhari.
TMA
imeeleza kwamba athari zinazoweza kutokea ni mafuriko ambayo
yatasababisha msongamano wa magari na watu hali itakayochelewesha
usafiri na usafishwaji maeneno ya mjini.
Aidha
kwa siku ya jana asubuhi kulikuwa na wingu zito lililoashirijia ujio wa
mvua kubwa, lakini haikunyesha mvua hiyo kama ilivyotarajiwa huku
asubuhi ya leo majira ya saa kumi na mbili asubuhi katika baadhi ya
maeneo jijini Dar es salaam imenyesha mvua ambayo imedumu kwa kipindi
kifupi.
0 comments:
Post a Comment