Halmashauri
ya jiji la Dar es salaam ipo kwenye majadiliano ya kuhamisha kituo cha
Mabasi yaendayo haraka Udart kilichopo jangwani na kuhamishia kituo cha
Mabasi yaendayo Mikoani Ubungo (UBT).
Hatua
hiyo ni kutokana na eneo hilo la jangwani kukumbwa na mafuriko ya mara
kwa mara hali inayosababisha kuharibika kwa magari hayo.
Kufuatia
kikao cha kawaida kilichofanyika jana cha Madiwani, Meya wa jiji la
Dar es salaam, Isaya Mwita amesema uamuzi huo umefikiwa kunusuru magari
hayo yasiendelee kuharika.
Menejimenti ya kampuni ya UDART na viongozi wa jiji wapo kwenye majadiliano kuhusu suala hilo waweze kufikia mwafaka.
”kwa
sasa tupo kwenye majadiliano kwa ajili ya kuhamisha kituo cha mabasi
yaendeyo kasi UDART cha Jangwani tuweze kukipeleka Ubungo kwa sababu
eneo la jangwani limekuwa likikumbwa na mafuriko ya mara kwa mara mvua
inapomyesha" alisema Mwita.
Alisema
suala hilo linaendelea kufanyiwa kazi na Halmashauri ya jiji hilo ipo
kwenye mchakato wa kupanua Mto Msimbazi uweze kuwa na nafasi kubwa ya
kusafirisha maji hadi baharini.
Kufuatia
mvua zilizokuwa zinaendelea kunyesha jijini Dar es salaam, Jangwani ni
moja ya eneo ambalo mara kwa mara limekuwa likikumbwa na mafuriko na
kupelekea safari za mabasi ya mwendokasi kuhairishwa
Aidha
kufuatia mvua zilizonyesha siku tatu zilizopita zimepelekea mabasi 29
kati 140 kuharibika na na kufanya baadhi ya wafanyakazi kupewa likizo
mpaka marekebisho yatakapokamilika.
0 comments:
Post a Comment