Mbunge
wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ali Mohamed Kessy amesema anao ushahidi wa
baadhi ya viongozi wakubwa waliomilikishwa miradi ya maji katika Mkoa wa
Rukwa namna wanavyomshawishi ili asizungumze kuhusu ubadhirifu uliopo
katika miradi hiyo.
Aidha,
alisema kutokana na wakandarasi kupewa miradi kimjomba mjomba
imesababisha wananchi wa Nkasi kukosa maji na kipindi cha masika
huchimba maji kwenye madimbwi kama panya.
Kessy
ametoa kauli hiyo jana Mei 8, bungeni jijini Dodoma wakati akichangia
bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji ambapo pamoja na mambo mengine
amesema viongozi hao wanapewa zabuni za miradi hiyo kiujanja ujanja.
“Awamu
ya nne mkandarasi alipewa mabilioni ya fedha, miaka kadhaa sasa bwawa
halina maji, wizara inaibiwa hela… na viongozi wakubwa ndiyo wenye
miradi, kwa ushahidi wananitafuta ili nizungumze nao nawakatalia, eti
mbunge nyamaza, ili waibe zaidi?” alisema.
Pamoja
na mambo mengine, alisema katika mkoa huo kumejitokeza ujambazi kwa
wakandarasi wa miradi ya maji katika baadhi ya vijiji vya Nkasi ambao
hata Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Isack Kamwelwe na Naibu wake, Juma
Aweso waliona namna serikali inavyoibiwa fedha.
“Mradi
wa Kamwala, mkandarasi ameingia mkataba wa Sh bilioni 7.7 wakati uwezo
mdogo, anao uwezo wa kutekeleza miradi ya thamani ya Sh 750 lakini
akapewa kijomba mjomba.
“Maelezo
bodi ya usajili wa wakandarasi yalieleza kuwa mkandarasi huyu hana
sifa, Baraza la Madiwani Nkasi lilimkatalia lakini akapewa kimjomba
mjomba,” alisema.
0 comments:
Post a Comment