Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA), imekamata malori mawili yenye bidhaa
mbalimbali eneo la Loliondo Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha kupitia
njia ya magendo yakitokea nchini Kenya zenye thamani ya zaidi ya
shilingi milioni 20.
Akizungumza
jana jijini Arusha, Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Charles Kichere alisema
kuwa, malori hayo yenye namba T 985 AJP na T 840 ABF yalikamatwa usiku
wa tarehe 10 Mei, 2018 na kusisitiza kuwa wafanyabiashara wenye bidhaa
hizo wamevunja sheria kwa kuwa hawakulipa kodi stahiki kama
inavyotakiwa.
Kichere
alifafanua kuwa, wafanyabiashara wenye bidhaa hizi zilizokamatwa,
wamevunja kifungu cha sheria namba 82 na 200 cha Sheria ya Usimamizi wa
Kodi ya Mwaka 2015 na Sheria ya Forodha ya Afrika Mashariki ya Mwaka
2004.
"Kwa
ujumla bidhaa hizi zote zina thamani ya shilingi 20,037,330.15 ambayo
kodi ya bidhaa hizi ni shillingi 28,524,758.11 na adhabu au faini ya
bidhaa hizi ni shilingi 10,768,665.08. Hivyo jumla ya mapato
yanayotakiwa kulipwa Serikalini ni shilingi 39,293,423.19," Kichere.
Ameongeza
kuwa "Hivyo kwa Sheria hizo, wafanyabiashara hawa wanatakiwa kulipa
kodi pamoja na faini ya shilingi milioni 39 na magari yao kutaifishwa".
Amezitaja
bidhaa zilizokamatwa kuwa ni pamoja na mifuko 362 ya sukari yenye uzito
wa kilo 50 kila mmoja, maboksi 40 ya mafuta ya kula yanayoitwa Karibu,
maboksi matatu ya mafuta ya kula yanayoitwa Daria, magaloni 100 ya
mafuta ya kula yanayoitwa Nyata na maboksi matatu ya viungo vya mboga
Kufuatia
tukio hilo, Kamishna Mkuu Kichere amewakumbusha wafanyabiashara wote
kuzingatia taratibu za uingizaji bidhaa nchini ili kuepuka hasara kwenye
biashara zao na kuongeza kuwa, TRA haitavumilia ukiukwaji wowote
utakaofanywa na wafanyabiashara kwa kutozingatia sheria na taratibu
hizo.
0 comments:
Post a Comment