Upande
wa utetezi katika kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi tisa wa
Chadema akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, umeomba
Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu kutupilia mbali mashtaka dhidi ya
washtakiwa kwa kuwa yanamapungufu, kisheria.
Maombi
hayo yamewasilishwa jana Mei 16, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,
Wilabard Mashauri na Wakili Peter Kibatala, ambaye aliwasilisha
mapingamizi nane ya kisheria ‘yanayoshambulia’ uhalali wa hati ya
mashtaka na mashtaka dhidi ya washtakiwa.
Katika
Mapingamizi hayo, Kibatala alidai, kibali cha DPP kina mapungufu ya
kisheria kwa sababu haioneshi imetolewa kwa mashtaka yapi na pia hati ya
mashtaka imewataja majina washtakiwa wote bila ya kufafanua na pia
imetaja tu kifungu cha sheria ambacho washtakiwa wameshtakiwa nacho huku
akidai pia kwamba, hakuna kibali kilichowasilishwa mahakamani hapo kwa
maana hiyo mashtaka dhidi ya washtakiwa yamepelekwa mahakamani hapo bila
ridhaa ya DPP.
Aidha,
Kibatala alitoa ombi mbadala na kuomba, iwapo mahakama itashindwa
kuifuta hati nzima ya mashtaka yanayowakabili washtakiwa hao basi
iyafutilie mbali mashtaka ambayo yanamapungufu kisheria, likiwamo shtaka
la nne, latano, la sita na la saba.
Alidai,
maelezo ya mashtaka hayo yanawachanganya washtakiwa na hawawezi
kujitetea ipasavyo, pia mashtaka hayo kufunguliwa kwake kunahitaji
ridhaa ya (DPP) ambayo haipo kutokana na mapungufu hayo, inaonesha
hakuna ridhaa yake.
“Kwa
kuwa mashtaka hayo tajwa kufunguliwa kwake kunahitaji ridhaa ya DPP,
lakini kuwa haipo tunaomba yafutiliwe mbali. Hati ya mashtaka
inamapungufu kwa sababu shtaka la pili na la tatu hayana maelezo ya
kutosheleza ya kuwapa washtakiwa msingi na uwezo wa kuweza kujitetea
kikamilifu katika kesi hiyo ya jinai.
“Katika
shtaka la kufanya mkusanyiko bila kibali hati haijataja watu
waliotishiwa na kwamba wametajwa kwa wingi hivyo haijulikani ni
washtakiwa ama ni watu wengine. Mashtaka yanayowakabili washtakiwa
yamejichanganya na hayaonyeshi walipelekeaje kifo cha Akwilina na hao
majeruhi walijeruhiwa na nani na kwa kutumia nini,” alisema Kibatala.
Amedai
maelezo katika hati ya mashtaka yamerundikana kiasi kwamba ni vigumu
mtu kujitetea na kwamba unapomshtaki mtu kwa kisababisha kifo ni lazima
utoe Maelezo ya kutosha kuonesha unamaanisha kitu Fulani ili mtu aweze
kujitetea.
Alidai
mapungufu mengine yaliyomo kwenye hati hiyo ni kuwa hayaoneshi dhumuni
la pamoja ambalo washtakiwa walikutana kulitenda hivyo linawanyang’anya
washtakiwa haki ya kujitetea. Kibatala alidai kuwa hati ya mashtaka
inamapungufu kwa sababu vifungu vilivyotajwa katika shtaka la Tatu, tano
na saba siyo sahihi.
Alidai
kuwa katika shtaka la kumi, kumi na moja na kumi na mbili yanamapungufu
kisheria kwa sababu hayaonyeshi watu waliochochewa kufanya makosa ni
wakina nani waliohudhuria mkutano, wakazi wa Kinondoni ama wapiga kura
bila kujali itikadi zao.
Akijibu
mapingamizi hayo, Wakili wa serikali Mkuu, Paul Kadushi aliiomba
mahakama kuyatupilia mbali mapingamizi yote hayo ya upande kwa kuwa
hayana mashiko kisheria.
Kuhusu
kibali cha DPP kinachoipa mahakama ridhaa ya kusikiliza kesi, Kadushi
alidai kuwa hakuna uamuzi wowote ulioweka msingi kwamba ni lazima kiwepo
na nini ama hakipaswi kuwepo.
Akiahirisha kesi hiyo, hakimu Mashauri alisema atatoa uamuzi kuhusu pingamizi hizo Juni 11, mwaka huu.
Mbali na Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa Chadema, washtakiwa wengine ni mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa; naibu katibu mkuu wa chama hicho Zanzibar, Salum Mwalimu; na wa Bara ambaye pia ni mbunge wa Kibamba, John Mnyika.
Wengine ni mbunge wa Tarime Mjini Esther Matiko; katibu mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji; mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche; mbunge wa Kawe, Halima Mdee na wa Bunda, Ester Bulaya.
Mbali na Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa Chadema, washtakiwa wengine ni mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa; naibu katibu mkuu wa chama hicho Zanzibar, Salum Mwalimu; na wa Bara ambaye pia ni mbunge wa Kibamba, John Mnyika.
Wengine ni mbunge wa Tarime Mjini Esther Matiko; katibu mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji; mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche; mbunge wa Kawe, Halima Mdee na wa Bunda, Ester Bulaya.
0 comments:
Post a Comment