Serikali
imesema itawalipa mawakala wote wa pembejeo za kilimo baada ya vyombo
vya uchunguzi kukamilisha uchunguzi wa watumishi waliodanyanga kuhusu
malipo na uhakiki wa madeni unaendelea.
Akijibu
baadhi ya hoja za wabunge waliozitoa wakati wakijadili bajeti ya wizara
ya kilimo ya mwaka 2018/19, jana jioni Mei 16, 2018, Naibu Waziri wa
Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji alisema malipo ni mara baada ya
uchunguzi kukamika.
“Nani
kaiibia Serikali, katika maombi haya vyombo vya uchunguzi vipo kazini,
sisi kama wabunge wasimamizi wa rasilimali, vyombo vya uchunguzi ni
muhimu na kama ni mtumishi nani aliongeza sifuri katika milioni 20 ikawa
bilioni, fedha si tatizo na tutawalipa wote wanaoidai Serikali,”
alisema Dk Kijaji
Kuhusu
kutengwa kwa bajeti kidogo, Dk Kijaji alisema Serikali inatambua
umuhimu wa sekta ya kilimo lakini utengaji wa bajeti unategemea
rasilimali zilizopo.
“Rasilimali
ziko chache kuliko mahitaji, sote tupo hapa, mlisema bajeti ya afya
iongezwe, maji iongezwe na ifahamike Serikali inatoa kipaumbele kwa
kilimo na sisi tunatambua kuwekeza katika kilimo,” alisema Dk Kijaji
Alisema
miongoni mwa jitihada hizo ni kuiwezesha Benki ya Kilimo: “Tumewekeza
Sh60 bilioni na mpaka sasa wana Sh66 bilioni, wameweza kuongeza kiwango
hiki katika utendaji wetu na tumechukua mkopo zaidi ya Sh250 bilioni na
kuipa benki hii.”
Akigusia
benki hiyo kuwa jijini Dar es Salaam, alisema mwezi huu itafungua tawi
jijini Dodoma, Juni jijini Mbeya na Julai jijini Mwanza na dhamira yetu
ni kuwafikia wananchi kule waliko.
Kwa
upande wake, Naibu waziri wa Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa (Tamisemi) Joseph Kakunda alitoa maagizo kwa maofisa kilimo
kutoka ofisini na kwenda kuelimisha wakulima na wale watakaoshindwa
watachukuliwa hatua.
“Lazima
wakulima wapate haki yao ya elimu kuhusu kilimo na utaratibu wa
kusubiri posho ili aende kufanya kazi yake tumeshapiga marufuku,”
alisema Kakunda.
Kakunda
alisema, “maofisa ushirika lazima wahakikishe wanafanya mapitio ya
vyama vya ushirika ili kujua kama utendaji ni mzuri na kama ni mbovu
wavifute na kuvisajili upya.”
“Maofisa
ugani wafanye kazi ya kuwatambua wakulima wote ili Serikali ifanye
maandalizi ya haraka ya kuandaa pembejeo, walio chini ya Tamisemi wapate
huko hizi taarifa na uzembe hautavumiliwa,” alisisitiza.
Kwa
upande wake, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso alisema
Serikali imetenga zaidi ya Sh29 bilioni kwa ajili ya kilimo cha
umwagiliaji na, “sisi kama wizara tutalisimamia hili na tunaahidi
kushirikiana vizuri na wadau wa wizara ya kilimo.”
0 comments:
Post a Comment