Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kuilinda na kuitunza
miundombinu ya Shirika la Umeme nchini (Tanesco), huku akiagiza mamlaka
husika kuwashughulikia watakaojihusisha na uharibifu wa miundombinu
hiyo.
Majaliwa
ameyasema hayo jana Mei 21, alipokuwa akizindua uunganishaji wa gridi
ya taifa kwa Mkoa wa Lindi na Mtwara iliyofanyika katika Kituo cha
kupozea umeme cha Maumbika mkoani hapa.
“Wapo
baadhi ya watu wasio na nia njema na serikali wanaharibu miundombinu
kwa kung’oa vyuma na kuuza kama vyuma chakavu, hawa ni wahujumu uchumi.
“Naagiza
mamlaka zinazohusika kufanya ukaguzi kila eneo linalouza au kununua
chuma chakavu kubaini kama kuna miundombinu ya Tanesco na endapo
mtaikuta wahusika wawajibishwe kwa mujibu wa sheria,” alisema Majaliwa.
Pamoja
na mambo mengine, Waziri Majaliwa amesema kuwa mkakati uliopo sasa ni
kuboresha miundombinu ya zamani na kujenga miradi mipya ya umeme ili
kuzalisha umeme wa kutosha ili kuwafikia wananchi wengi.
0 comments:
Post a Comment