Serikali
imesema hali ya ukame uliozikumba nchi za ukanda wa Mashariki, Kati na
Kusini mwa Afrika mwaka 2017/18 umesababisha Tanzania kushindwa kufikia
matarajio ya sukari tani 314,000 na badala yake imezalisha tani
300,399.
Akiwasilisha
bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na uwekezaji ya mwaka 2018/19,
waziri wa wizara hiyo, Charles Mwijage amesema takwimu hizo ni za hadi
kufikia Aprili 20, 2018.
Amesema
mahitaji ya sukari nchini ni takribani tani 630,000 kwa mwaka na kwamba
kati ya kiasi hicho tani 485,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na
tani 145,000 ni kwa ajili ya matumizi ya viwandani.
“Sukari
kwa matumizi ya viwandani haizalishwi hapa nchini. Uwezo wa uzalishaji
wa ndani kwa sasa ni wastani wa tani 320,000 kwa mwaka. Pengo la
mahitaji takriban tani 165,000 za sukari ya kawaida na tani 145,000 za
viwandani huzibwa kwa kuagizwa kutoka nje ya nchi,”amesema.
Amesema
kampuni nne zinayozalisha sukari nchini ndizo zilizopewa jukumu la
kuagiza sukari kwa masharti kuwa hakutakuwa na upungufu wa sukari
nchini na ni lazima wapanue mashamba ya miwa ili ifikapo mwaka 2020
Tanzania ijitosheleze kwa sukari.
Amezitaja kampuni zilizopewa jukumu la kuagiza sukari kutoka nje ya nchi kuwa ni Kilombero , TPC, Kagera na Mtibwa.
0 comments:
Post a Comment