Mbunge
wa Muleba Kusini(CCM), Profesa Anna Tibaijuka ameitaka serikali ya
awamu ya tano iwajibike kuwanunulia ng'ombe wafugaji walioshinda kesi
zao Mahakamani kama sheria inavyosema nasio vinginevyo.
Prof.
Tibaijuka ametoa kauli hiyo jana Mei 22, 2018 Bungeni Jijini Dodoma
kwenye kikao cha 34 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Maliasiri na Utalii
ya mwaka 2018/19 ambayo ni shilingi 115.8 bilioni baada ya kuwepo tatizo
la muda mrefu kwa wafugaji kuporwa mifugo yao na watu wa maliasili
pindi wanapokuwa wamevamia hifadhi kwa lengo la kulisha mifugo yao.
"Serikali
hii ya awamu ya tano naishukuru sana walitoa miezi 10 kwa Mawaziri humu
ndani Bungeni kutafuta ardhi za wafugaji lakini hiyo kazi haikufanyika
kilichotokea watu walikuja kuondolewa kwenye hifadhi kama operesheni na
kwa kweli yalikuwa mateso makubwa sana. Mhe. Spika ni utawala wa sheria
kama mtu ameshinda mahakamani na anatakiwa arudishiwe mifugo yake ni
lazima afanyiwe hivyo na kama haipo lazima inunuliwe, serikali hapo
inatakiwa kuwajibika", alisema Tibaijuka.
Pamoja
na hayo, Prof. Tibaijuka aliendelea kwa kusema "kuwajibika hakuwezi
kuwa sehemu ya wananchi pekee yake bali na serikali yenyewe lazima
iwajibike pale ambapo kosa limefanywa na watendaji wake".
Kwa
upande mwingine, Profesa Anna Tibaijuka amesema hawezi kuiunga hoja
iliyokuwa mezani mpaka pale suala lake litakapopatiwa majibu yenye
kuridhisha.
0 comments:
Post a Comment