Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa ajira zinazotolewa kwa wageni ni zile Kitaalum tu ambazo Watanzania hawana uwezo nazo.
Waziri
Mkuu ameyasema hayo leo Mei 17, wakati wa kipindi cha maswali na majibu
kwa Waziri Mkuu ambapo pamoja na hayo ameelza kuwa wataendelea
kusimamia na kuhakikisha kwamba Watanzania wanapata fursa namba moja ya
kuajiriwa.
“Serikali
imeratibu vizuri sana suala la ajira nchini, na imetoa kipaumbele kwa
Watanzania kupata ajira kwenye sekta zote nchini, wageni wanazo fursa
lakini kwa masharti, ajira za wageni zote nchini ni nafasi za kitaalamu
tu ambazo Watanzania hawana uwezo nazo,” amesema Waziri Mkuu.
Aidha
ameongeza kuwa serikali itaendela tutaendelea suala la ajira na
kuhakikisha kwamba Wtanzania wanakuwa namba moja katika kuajiriwa katika
sekta zote ndani ya nchi.
0 comments:
Post a Comment