WATUMISHI
wa Afya wa ngazi ya Jamii,Zahanati , Vituo vya afya vya na Hospitali za
Kliniki za Mama na Mtoto za Wilaya zinatakiwa kuchunguza Uakisi wa
mwanga kwenye mboni za watoto kila wanapoenda kucheki ukuaji wa watoto
hao ili kupunguza uwepo wa saratani ya macho kwa watoto.
Hayo
yamesemwa na Mganga Mkuu wa Serikali ambaye ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara
ya Afya Prof. Mohammed Bakari Kambi wakati akitoa tamko la saratani ya
macho kwa watoto kwa niaba ya Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,
Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katika ofisi ndogo za Wizara Jijini
Dar es salaam.
“Iwapo
mtoa huduma za afya unahisi kuwa mtoto ana tatizo kwenye jicho
usimrudishe nyumbani hadi uhakikishe mtoto huyo ameonwa na mtaalamu wa
macho ili kugundua kama ana tatizo kwenye macho yake” alisema Prof.
Kambi.
Aidha
Prof. Kambi amesema kuwa katika kuboresha huduma hizo Wizara imeandaa
mwongozo ambao utasaidia kuinua uelewa wa wataalamu wa afya ili waweze
kuwatambua watoto wenye tatizo hilo na kuwapa rufaa mapema.
Kwa
Mujibu wa Prof. Kambi amesema kuwa takwimu za hapa nchini zinaonesha
kuwa watoto137 wenye saratani hii walionwa kwenye vituo vya kutolea
huduma za afya kwa mwaka 2017 na watoto 80 hadi 100 hupewa rufaa na
kufika kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na wengine hutibiwa KCMC
Moshi.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi wa mpango wa Macho wizara ya Afya Dkt.
Benadertha Shilio amesema kuwa anawashukuru wadau wote wa macho ambao
wamekuwa bega kwa began a Serikali ya Tanzania katika kufanikisha
kuboresha huduma za Macho kwa watoto.
“Tunawashukuru
Rotary Club ya Dar es salaam Oysterbay wakishirikiana na Rotary Club ya
Chelsea nchini Uingereza ambao wametoa msaada wa vifaa mbalimbali vya
kutibu Saratani ya macho vinavyogharimu kiasi cha Dola za Kimarekani
65,000 na Kampuni ya Pricewaterhouse ya Tanzania ambayo imetoa vifaa
vyenye thamani ya shilingi milioni 25 ambavyo vimesambazwa Muhimbili na
Mloganzila” alisema Dkt. Shilio.
Maadhimisho
ya Wiki ya sarani ya Macho kwa watoto kwa mawaka 2018 imebeba kauli
mbiu isemayo “MBONI NYEUPE KWENYE JICHO LA MTOTO INAWEZA KUWA SARATANI
YA MACHO”.
0 comments:
Post a Comment