Waziri
wa Mambo ya Ndani, Dkt. Mwigulu Nchemba ameagiza jeshi la Polisi nchini
kuruhusu Taasisi za dini kufanya mikutano yao watakapoomba kibali.
Aidha,
amesema ni lazima kuheshimu uhuru wa kuabudu wa kila dini uzingatiwe
kwa kuruhusu wanafunzi na wafanyakazi kwenda sehemu zao za kuabudu kama
ilivyopangwa.
Akizungumza
katika kongamano lililoandaliwa na Kanisa la Waadventista Wasabato
jijini Mwanza, Dkt. Mwigulu alisema kuwa mafundisho yanatotolewa na
taasisi za dini yanasaidia kuwa na jamii yenye raia wema.
Alisema
kwa kuwa Wizara hiyo ndiyo yenye mamlaka ya kusimamia uhuru wa kuabudu,
watahakikisha wanazungumza na mashirika n ahata shule ambazo zinawazuia
wanafunzi na wafanyakazi kuhudhuria kwenye ibada siku za jumamosi.
‘’Nimeagiza
jeshi la Polisi wawape uhuru wa kuabudu kwa sababu mnatengeneza jamii
iliyobora lakini pia tutazungumza na wahusika kwenye taasisi za elimu na
ajira ili tutoe maamuzi yatakayotolewa yasilete doa kwani kazi hii
inasaidia kunyoosha nchi,’’ alisema Dk Mwigulu.
Naye,
Katibu Mkuu wa Kanisa hilo Kanda ya Nyanza Kusini, Steven Swita alisema
kuwa kumekuwa na changamoto ya waumini wa kanisa hilo kuzuiliwa kwenda
kuabudu siku ya jumamosi kulingana na imani zao.
‘’Kumekuwa
na utaratibu wa kupangwa masomo ya ziada na mitihani siku ya jumamosi
pamoja na udahili wa wafanyakazi na wasipohudhuria huadhibiwa kwa viboko
kwa wanafunzi wa shule za msingi na wale wa elimu ya juu wanafukuzwa
shule,’’ alisema Swita
0 comments:
Post a Comment