Naibu
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso amewatahadharisha watumishi
wote waliokuwa chini ya Tamisemi katika miradi ya maji ambao wamehamia
Wizara ya Maji kwamba wanatakiwa kunyooka vinginevyo watanyooshwa.
“Nimshukuru
sana Mheshimiwa Rais John Magufuli kwa kutoa agizo la watumishi wote wa
sekta ya maji kuwa chini ya Wizara yetu, nawatahadharisha kuwa lazima
waje wakiwa wamenyooka na kama watashindwa sisi tutawanyoosha,’ amesema
Aweso.
Aweso alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Mbarala, Haroon Mulla Pirmohamed bungeni leo Mei 14.
Pirmohamed
alitaka kujua ni lini Serikali itamaliza kujenga skimu za umwagiliaji
Ipatagwa, Kongoro/Mswiswi, Motombaya na skimu mpya ya Mhwela mpaka
Kilambo.
Naibu
Waziri amesema katika mwaka wa fedha 2017/18, Serikali kupitia
halmashauri ya Mbarali ilitumia kiasi cha Sh 20 Milioni kwa ajili ya
kufanya ukarabati mdogo wa banio la Igumbilo lililopo Kata ya Chimala
ili kuwawezesha wakulima kuendelea kutumia banio hilo kwa shughuli za
umwagiliaji kwa muda.
0 comments:
Post a Comment