Muigizaji
wa Bongo movie Wema Sepetu ameendelea kuwa na mwezi mzuri kwani siku
chache baada ya kupata ubalozi wa Kombe la Dunia na Star Times siku ya
jana Wema alilamba dili nono na Tatu Mzuka.
Siku
ya jana Kampuni ya The Network ambayo inahusika na kuendesha Michezo ya
namba ya Tatu mzuka, imetangaza kuingia kwenye ushirikiano wa
kibiashara na Wema.
Akizungumza
Kwenye mkutano na waandishi wa habari, mkuu wa kitengo cha mawasiliano
wa Tatu Mzima Sebastian Maganga, alisema ushirikiano wao na Wema ni
mpango mkakati wa Tatu Mzuka wa kufanya kazi bega kwa bega na Watanzania
ili kuboresha maisha yao.
"Kusudi
kubwa la Tatu Mzuka kuingia makubaliano na Wema, ina lengo la kutaka
kusambaza fursa kwa watu wengi kadri iwezekanavyo ili kuboresha maisha
yao ya kila siku”.
Lakini pia Wema aliyepata shavu hilo alifunguka na kusema:
"Nina
hamu kubwa ya kuanza kuwashirikisha bidhaa hii mashabiki zangu wote na
Watanzania kwa ujumla wao ili waweze kujitengenezea fursa nyingi za
kuboresha maisha yao kupitia kwangu."
0 comments:
Post a Comment