Msanii wa muziki Rehema Chalamila a.k.a Ray C usiku wa jana alikamatwa na jeshi la polisi maeneo ya Kinondoni Manyanya almaarufu ‘Kinondoni kwa Mpemba’ jijini Dar es salaam baada ya kuzidisha madawa ya kulevya na kuanza kupiga makelele barabarani akidai anataka kutekwa huku akitishia kuvua nguo.
Habari zinadai kuwa mama yake mzazi amekuwa akikesha kumtafuta mrembo
huyo kutokana na kuzama kwenye vijiwe vya mateja wa madawa hayo na
kushindwa kuonekana nyumbani.
Sambamba na hilo siku za hivi karibuni mwanamuziki Jay Dee, alionekana
kuwa naye karibu na kudai kuwa Ray C, anahitaji marafiki wazuri na watu
wavumilivu kuweza kumsaidia kwani kumlaumu pekee hakuwezi kumjenga bali
ni kuzidi kumharibu kisaikolojia.
Mmoja wa wasanii wa Bongo Movie, Esha Buheti, kupitia mtandao wa kijamii
ameweza kueleza jinsi gani alivyoguswa baada ya kumuoa Ray C akiwa
chini ya ulinzi wa polisi akiwa hajitambui na kuongea maneno
yasiyoeleweka na kudai kuwa awali alijua mrembo huyo anasingiziwa tuu.
Ameandika “Nashindwa hata niongee nini jamani, Ray C leo Kinondoni
umenitoa machozi, jamani tufanye kitu tumsaidie Ray C, I mean it jamani
siku zote nlikuwa najua anaonewa ila nilichokishuhudia leo nimeumia
kutoka moyoni amedhalilika mwanamke mwenzetu, jamani tufanyeje?”
Akaendelea “Nilikua na Kabula, Kinondono kwa wapemba tumefuata chips
mara tukasikia mtu anasema me Ray C nataka kuvua nguo, nikajua utani
kushuka ni Ray C anasema nishikeni kuna watu wanataka kuniteka, alikuwa
na nguvu sana watu kumshika akaanza kuongea vitu havieleweki, akaanza
kutafuta kisu ajichome, watu walimzuia sana walishindwa akaanza
kugaragara kwenye matope akipiga kelele,”
“Kiukweli nilijikuta nalia mara ikaja gari ya polisi ikambeba ila kwa
tabu sana alikua akipiga kelele jamani nisaidieni msiniache kiukweli
mpaka Ray C anaondoka na ile gari ya polisi sikujua anapelekwa wapi
alikuwa kama mtu alopata kichaa, YARRAB TUNAMSAIDIAJE RAYC?”.
Baada ya ujumbe huo, aliamua kupost video tena na kuandika:
"Ray C hastahili haya jamani kweli Leo hii anafikia hatua hii? Najua hajitambui ila tumfikirie mwanamke mwenzetu ambae ni mamaake, anajiskiaje? Rayc nn kimekupata ? Hiii video inasambaa kila sehem kweli huyu ndo RAYC AMBAE NI NEMBO YA TAIFA? Plz tumsaidie manake tusimhukumu? MBONA sisi kila siku mungu tunamkosea na hesabu makosa yetu?
"Ray C hastahili haya jamani kweli Leo hii anafikia hatua hii? Najua hajitambui ila tumfikirie mwanamke mwenzetu ambae ni mamaake, anajiskiaje? Rayc nn kimekupata ? Hiii video inasambaa kila sehem kweli huyu ndo RAYC AMBAE NI NEMBO YA TAIFA? Plz tumsaidie manake tusimhukumu? MBONA sisi kila siku mungu tunamkosea na hesabu makosa yetu?
"We
need to do something jamani @tzshaderoom @mangekimambi_ @divathebawse
@babutale @ @mwanafa @linexsundaymjeda @paulmakonda naomba tumstiri huyu
mtu plz plz @lisa_fickenscher ( tunafanyaje kumsaidia jamani tusichoke
me natamani aende rehab mwaka mzima)
"Leo
rayc umedhalilika najua haikua akili yako mama DAAAAH hata sijui
amepelekwa wapi maskini 😢😢 atakua amelala wapi? Vipi kuhusu kesho
Yake? Mamaake anajiskiaje?
"Inaumaa
jamani tusikubali kumpoteza huyu dada nawaombaa 🙏🙏🙏 tusaidiane
@rayc1982 my love kama hauko sawa jamani ongea na watz wapo tayari
kujitolea kwa hali na mali my love"