Leo
June 17 2016 idadi ya wabunge kusimamishwa imeongezeka baada ya Naibu
Sika, Tulia Ackson kutangaza kusimamishwa kwa wabunge wawili ambao ni
Mbunge wa viti Maalum CHADEMA Suzan Lyimo na Anatropia Theonest.
Mbune
Suzan Lyimo amesimamishwa na Bunge kuhudhuria vikao vitano vya Bunge
baada ya kubainika kusema uongo kwamba Jeshi la polisi nchini limenunua
magari 777 ya washawasha wakati ukweli ni kwamba hiyo ni Idadi ya magari
inayopangwa kuingizwa na jeshi hilo kwa ajili ya matumizi mbalimbali.
Licha
ya Mbunge kuonesha ushirikiano kwa kamati ya maadili, haki na madaraka
ya bunge, kamati imemwona Mbunge ni mzoefu wa shughuli za bunge hivyo
anapaswa kusimamishwa vikao hivyo kuanzia June 17 hadi 24 mwaka huu.
Aidha
Mbunge Anatropia Theonest amesimamishwa kuhudhuria vikao vitatu vya
bunge kwa kosa la kulidanganya Bunge kuwa waziri wa ardhi na nyumba
William Lukuvi alichukua ardhi ya wananchi akiwa mkuu wa mkoa wa Dar es
salaam.