SERIKALI
imekusudia kutunga sheria ya kupiga marufuku ajira za wasichana wa kazi
wenye umri chini ya miaka 18 kabla ya mwisho wa mwaka 2016.
Hatua
hiyo inaelezwa inakusudia kuinua hadhi ya kazi na ajira za wasichana
wa kazi nchini, kwani muda wa kurasimisha ajira hizo umefikia wakati
wake.
Hayo yamebainishwa jana mjini Dodoma
na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.
Ummy Mwalimu wakati akizungumzia na waandishi wa habari kuhusu
maadhimisho ya siku ya mtoto wa afrika inayoadhimishwa tarehe 16 Juni
kila mwaka.
Alisema
hatua inachuliiwa na Serikali kutokana na wasichana wengi wa ndani
kutumikishwa kazi hiyo katika umri mdogo na kulipwa ujira mdogo.
“Tumepanga
kutunga kanuni na sheria ya kupiga marufuku ajira za wasichana wa kazi
wenye umri chini ya miaka 18, na ndio maana tunawachukua katika umri
mdogo sana na kuwalipa ujira mdogo, hivyo ukimchukua binti wa miaka 18
utaweza kuinua hadhi ya kazi ya kazi yenyewe” alisema Waziri Ummy.
Akizungumzia kuhusu maadhimisho hayo, Waziri Ummy aliitaka jamii kukataa kurubuniwa kwa pesa na katika kuwafichua
watu wanaofanya vitendo vya ukatili kwa watoto ikiwemo kulawiti na
kuwabaka na badala yake watoe taarifa katika vyombo vya dola ili adhabu
kali zichuliwe dhidi yao.
Aidha
Waziri Ummy aliwata wazazi nchini kujenga tabia ya kukagua maumbile ya
watoto wao hususani watoto wa kike ikiwemo kuwaogesha angalau mara moja
kwa mwezi, kwani kwa kufanya hivyo kutamwezesha mzazi kufahamu afya ya
kimwili ya motto wake.
Kwa
mujibu wa Waziri huyo alisema vitendo vya ulawiti havifanywi kwa watoto
wa kike pekee bali na watoto wa kiume pia wamekuwa wahanga wa vitendo
hivyo, ambapo ameitaka jamii kutowaamini ndugu au jamaa zao kulala
kitanda chumba kimoja na watoto wao.
“Kwa
mujibu wa taarifa za jeshi la Polisi, vitendo hivi vimekuwa vikifanyika
zaidi majumbani kwa asilimia 49, asilimia 23 wakati wa kurudi na
kwenda shule na asilimia 15 wakiwa shuleni, hivyo kwa takwimu hizi
unaweza kuona ukubwa wa tatizo ulivyo” alisema Waziri Ummy.
0 comments:
Post a Comment