test

Monday, June 20, 2016

Wataalamu wa Prescion Air na TCAA Waelekea Zanzibar Kuchunguza Tukio la Ndege Kuwaka Moto


Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), wakishirikiana na mafundi wa Kampuni ya Ndege ya Prescion Air wameelekea Zanzibar kuchunguza tukio la ndege ya kampuni hiyo kupata hitilafu na kuwaka moto na kusitisha safari.


Tukio hilo lilitokea Juni 16 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Karume mjini Zanzibar. 

Taarifa iliyotolewa jana na Mkuu wa Mawasiliano wa Prescion Air, Azda Mkullo inasema wamepeleka injini mbadala kwa ajili ya kufungwa.

Inaongeza kuwa baada ya tukio hilo ilimlazimu rubani kuchukua hatua za kuuzima moto na kuirudisha ndege kwenye eneo la maegesho. 

Ndege hiyo wakati ikipata hitilafu ilikuwa imefanya safari zake kati ya Kilimanjaro na Dar es Salaam.Ndege hiyo PW432 ilikuwa na abiria 34 na wahudumu wanne wote walitoka salama.
TANGAZA HAPA KWA BEI NAFUU