Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
amesema upimaji wa Kifua Kikuu (TB) na Ukimwi kwenye baa hautakuwa wa
lazima.
Akizungumza
wakati wa maadhimisho wa miaka 30 ya Mpango wa Taifa wa Kudhibiti
Ukimwi (NACP), Mwalimu alisema baada ya kutolewa taarifa ya kuwapo
mpango huo watu wengi wamekuwa na hofu.
“Tutatekeleza
mpango wa kusogeza huduma za upimaji TB na ukimwi kwenye baa, ila
hautakuwa wa lazima, tutachofanya ni kuwashawishi wananchi kutumia fursa
ya kusogezewa huduma hiyo,”alisema.
Aidha,
alisema kwa sasa wizara yake iko katika mkakati wa kufanyia marekebisho
ya Sheria ya Ukimwi kwa lengo la kuruhusu watu kujipima mwenyewe, kutoa
fursa kwa vijana kuanzia miaka 15 kwenda kupima ukimwi bila kupata
ridhaa ya wazazi au walezi.
“Haya
ni maeneo ambayo kama tutayafanyia marekebisho tutaweza kusaidia
kuongeza kasi ya kudhibiti maambukizi ya Ukimwi,” alisema.
Katika
hatua nyingine, Mwalimu aliagiza kuanzia Julai mosi mwaka huu, watu
wanaoishi wa virusi vya Ukimwi kupewa dawa za miezi mitatu badala ya
sasa ya kupewa kwa miezi mwili.
Agizo
alilitoa kutokana na Mwenyekiti wa Baraza la Watu wanaoishi na Virusi
vya Ukimwi, Justin Mwinuka kudai kuwa utaratibu wa kupewa dawa za miezi
miwili umekuwa ukiongezea gharama, kwani wamekuwa wakitakiwa kupima afya
zao kila baada ya miezi mitatu.
Waziri
huyo alisema utaratibu huo wa kuwapa dawa kwa miezi mitatu mitatu uanze
haraka isipokuwa kwa wale ambao wanaonekana hawataweza kutunza dawa
hizo au ambao ndio kwanza wanaanza kutumia dawa hizo.
0 comments:
Post a Comment