Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ‘NSSF’ Prof. Godius Kahyarara
ameeleza mapato yaliyopatikana kwenye daraja la Nyerere tangu
lilipofunguliwa rasmi May 14 2016.
Prof
Kahyarara amesema jumla ya shilingi bilioni 1.3 zimekusanywa kutoka
Daraja hilo lililopo Kigamboni jijini Dar es Salaam kupitia tozo
mbalimbali zinazolipwa na vyombo vya usafiri vinavyopita darajani hapo.
Prof.
Kahyarara ameongeza kuwa fedha hizo zimekusanywa kupitia tozo za magari
yakiwemo magari binafsi, magari ya abiria, magari ya mizigo, pikipiki
na bajaji zinazopita darajani hapo kila siku.
Kwa
upande wake Msimamizi wa Mradi wa Daraja la Nyerere, Bw. Gerald Sondo
alisema kuwa Serikali kwa kushirikiana na uongozi wa daraja wana mpango
wa kuboresha huduma za malipo ili watumiaji wa daraja hilo waweze kulipa
tozo kwa kutumia kadi za kielektroniki………
“Hivi
karibuni tunatarajia kuanzisha mfumo wa malipo kwa kutumia kadi za
kielektroniki ambapo madereva wa vyombo vya usafiri watakuwa wanatumia
kulipa tozo pindi wanapopita darajani”
Aidha
alisema kuwa kwa sasa idadi ya magari, pikipiki na bajaji zinazopita
darajani hapo ni kati ya elfu 8 hadi elfu 10 kwa siku na wanalipa tozo
kulingana na aina ya chombo cha usafiri.
Akieleza
kuhusu usalama wa daraja na watumiaji wake, Sondo alisema kuwa ulinzi
ni wa uhakika kwa saa 24 kila siku kwani kuna askari wa kutosha pamoja
na kamera zinazosaidia zoezi hilo pia kuwa wanaandaa kanuni za matumizi
ya daraja ikiwemo faini za uharibifu, uchafuzi wa mazingira, matumizi
mabaya ya njia na lugha za matusi.