Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan
amesema ukuosefu wa fedha, taarifa pamoja na ujuzi wa kukabiliana na
mabadiliko ya tabia nchi ni vikwazo vinavyoendelea kuongeza umaskini
nchini ambapo wanawake ndio waathirika wakubwa.
Mama
Samia aliyasema hayo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizindua mradi wa
Green Voices ambao unakusudia kuwasaidia wanawake katika kupambana na
mabadiliko ya tabia nchi ambapo wamegeuza changamoto kuwa fursa.
“Wote tumeshuhudia jinsi Bara la Afrika linavyopoteza mabilioni ya shilingi kila mwaka kutokana na mabadiliko ya tabia nchi”. Alisema Mama Samia.
Awali
Rais wa Mfuko wa Wanawake Afrika Mama Maria Terezo la Vega Fernandes
alisema atahakikisha anatimiza dhamira yake ya kuendelea kuwasaidia
wanawake wa Tanzania na Afrika katika maeneo ya kilimo, afya, Amani na
haki za binadamu.
“
Miradi ya Green Voices imeanzishwa katika nchi mbalimbali duniani kwa
lengo la kuwawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi na kujiletea maendeleo
yao”. Alsema Mama Tereza.
Naye
mjumbe wa Bodi ya ushauri wa mradi huo Balozi Getrude Mongela
alimpongeza mama Tereza kwa juhudi zake za kuwaunganisha wanawake katika
kuleta maendeleo na ukombozi wao kwa ujumla.
“Mradi
wa Green Voices umenikumbusha maazimio ya mkutano wa Reo De Jenairo
uliofanyika mwaka 1992, mkutano wa Cairo na Beijing ambayo ilizingatia
ushirikishwaji wa wanawake katika suala zima la mazingira”. Alisema Balozi Mongela.
Naye
mratibu wa mradi huo nchini Bi.Sechelela Balisydia amesema wanawake 15
kutoka Tanzania walipata mafunzo ya jinsi ya kukabiliana na mabadiliko
ya tabia nchi na uongozi nchini Spain.
Aliongeza
kuwa baada ya mafunzo hayo wameweza kutoa kutoa mafunzo kwa wenzao 250
kwa kuwashirikisha katika miradi ya ufugaji nyuki, mitambo ya kukaushia
mboga inayotumia nishati ya jua na kilimo cha uyoga.
Miradi
hiyo ipo katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Kigoma, Mwanza, Morogoro
na Kilimanjaro ambapo mradi huo mpaka sasa umetimiza mwaka mmoja