Chama
cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Kijamii nchini 'Tanzania
Bloggers Network' (TBN) kinasikitishwa na kulaani vitendo vya baadhi ya
Vyombo vya Habari kutumia kazi za wanachama wake (picha, video, habari)
bila idhini na bila kutoa maelezo stahiki ya vyanzo vya kazi hizo.
Mfano
mmoja ni Gazeti la kila siku la Majira, toleo namba 8217 la Alhamisi
Julai 7, 2016 ambalo bila aibu lilichukua picha katika Mtandao wa
Michuzi Blog ina kuitumia pamoja na malezo yake bila ridhaa wala kutoa
kueleza chanzo cha hiyo picha.
Vile
vile Wahariri wa Majira kwa makusudi waliondoa alama maalum ya
kumbukumbu iliyowekwa katika picha hiyo (watermark-logo) na kuichapisha
katika ukurasa wa mbele wa gazeti hilo, bila kutaja chanzo chake, jambo
ambalo ni ukiukwaji wa Sheria na kinyume na taaluma ya habari.
Kitendo
hicho ambacho pia kimekuwa kikifanywa na baadhi ya magazeti hapa nchini
kimeonesha dhahiri ni jinsi gani baadhi ya vyombo vyenye tabia hiyo
visivyothamini kazi za ‘bloggers’ na mchango wake kwenye tasnia nzima,
huku wakiendelea kulea waandishi na wapiga picha wavivu na wazembe
wanaotumia blogs kama njia ya mkato kupata material.
TBN
inatambua wazi si vibaya vyombo vya habari kutegemeana/kushirikiana kwa
kutumia kazi za chombo kingine lakini ni vema chombo kinachotumia kazi
ya mtu mwingine kumtambua kwa kumtaja katika kazi hiyo ama kukubaliana
na chombo husika kabla ya kufanya hivyo.
Chama
cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Kijamii nchini hakitafumba
macho kuona kazi za wanachama wake zikitumiwa na vyombo vingine vya
habari bila utaratibu na wala makubaliano ya kabla kwa wahusika.
Imetolewa na:-
Kamati ya Uongozi TBN Taifa,
Tarehe: 11/07/2016,
Dar es Salaam.
Tarehe: 11/07/2016,
Dar es Salaam.