test

Friday, July 8, 2016

Diamond, AY, Alikiba, Joh Makini, Yamoto Band, DJ D-Ommy watajwa kuwania tuzo za AEA Marekani,Fahamu vipengele wanavyowania


Diamond Platnumz, AY, Alikiba, Joh Makini na DJ D-Ommy na wengine wametajwa kuwania tuzo za Afrika Entertainment Awards, USA.
Ni Diamond ndiye aliyetajwa kuwania vipengele vingi zaidi vikiwemo Best Male Single, Best Video of The Year, pamoja na People’s Choice. AY na Alikiba wanawania kipengele kimoja cha Best Collaboration kwa nyimbo Zigo Remix na Nagharamia.
Joh Makini anawania vipengele viwili, Best Hip hop Artist na Best Video of the Year kwa wimbo wake Don’t Bother. Achia Body ya Ommy Dimpoz inawania pia kipengele hicho.
Vanessa Mdee anawania tuzo ya Best Female Single kwa wimbo wake Never Ever, Linah kipengele cha Best Female Artist, Yamoto Band – Hottest Group.
Vijana wa WCB Harmonize na Raymond nao wametajwa kuwania Best New Artist na Best New Talent (respectively).
DJ D-Ommy wa Clouds FM ni dj pekee wa Tanzania aliyetajwa kuwania kipengele cha Best DJ huku Millard Ayo akitajwa kuwania kipengele cha Best Blogger.
Kuwapigia kura watanzania waliotajwa bonyeza hapa.
Tuzo hizo zitatolewa October 22, New Jersey Marekani
TANGAZA HAPA KWA BEI NAFUU