Rais John Magufuli, amekataa kuwapandisha vyeo maofisa 17 wa polisi waolipendekezwa na amewapa nafasi ya kujipanga zaidi.
Rais Magufuli aliwapandisha vyeo maofisa 60 kuanzia Jumamosi iliyopita, kati yao 25 kutoka cheo cha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) kuwa Naibu Kamishna wa Polisi (DCP).
Wengine 35 aliwapandisha kutoa cheo cha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi.

Akizungumza
jana muda mfupi baada ya maofisa hao kuapa kiapo cha maadili ya umma,
Rais Magufuli alisema waliokuwa makamishna wasaidizi waandamizi
waliopelekwa kwake katika mapendekezo walikuwa 31, lakini wamerudi 25.
Pia, alisema waliokuwa makamishna wasaidizi wa polisi waliopendekezwa kuwa makamishna wasaidizi waandamizi wa polisi walikuwa 46, “ wamerudi 35.”
Pia, alisema waliokuwa makamishna wasaidizi wa polisi waliopendekezwa kuwa makamishna wasaidizi waandamizi wa polisi walikuwa 46, “ wamerudi 35.”
“Wale
ambao hawakurudi tuwape nafasi ya kujipanga tena zaidi. Nataka
niwaeleze ukweli kwa sababu inawezekana wako wengine walisikia kwamba
majina yao yalipelekwa…Sasa mkawaambie hayakurudi kwa sababu yangu. Wala wasihangaike kutafuta mchawi,” alisema Rais Magufuli.
Alisema
baada ya kupata taarifa na data zote walizonazo, “Nikaona tuwape muda
wa kujirekebisha. Kwa hiyo nyinyi mliofanikiwa mpaka mmefikia hapa
nawapongeza sana. “Mchakato ulikuwa mrefu na mzito,” alisema Rais
Magufuli.
Aliongeza,
“Nyinyi sasa ni makamanda tunaowategemea katika nchi hii.
Mmechaguliwa siyo kwa makosa. Mnastahili. Katekelezeni wajibu wenu bila
woga kwa kuzingatia sheria.”
Kuhusu
mchakato huo, Rais Magufuli alisema alimwagiza, IGP Ernest Mangu karibu
miezi mitano iliyopita
kuanza mchakato huo.
Alisema mchakato ulianzia na ukapita kwa wakuu wao (wa polisi) kwa kuangalia historia za wale ambayo majina yao yalikuwa pamoja na kazi zao.
Alisema mchakato ulianzia na ukapita kwa wakuu wao (wa polisi) kwa kuangalia historia za wale ambayo majina yao yalikuwa pamoja na kazi zao.
“Wakapita
(majina ya wapendekezwa) mahali pengine mpaka yamefikia
kwangu…Ninajua hamtaki kusema lakini mimi nimeumbwa kusema ukweli.”
Watumishi
‘raia’ kuondolewa
Katika hotuba yake ya takriban dakika 30 aliyotoa bila kusoma popote, Rais Magufuli alisema inawezekana wapo watendaji wachache ndani ya Jeshi la Polisi ambao aidha kwa makusudi au kwa nia yao mbaya wanalichafua jeshi hilo.

“Ninawaomba
mkawashauri na kuwaelekeza, ikishindikana mkawaondoe katika Jeshi la
Polisi. Mfano mzuri ni mhasibu ambaye aliorodhesha watumishi ambao si
maaskari kulipwa pensheni wanayolipwa maaskari.
“Mtu mwenyewe siyo askari, la kujiuliza nyinyi lakini mmeshindwa kumshika,” alihoji.
“Mtu mwenyewe siyo askari, la kujiuliza nyinyi lakini mmeshindwa kumshika,” alihoji.
Mhasibu
huyo, Frank Msaki (ambaye si polisi) alisimamishwa kazi na Katibu Mkuu
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira,
kwa makosa ya kufanya malipo hewa ya posho ya chakula kwa watu wasio
askari.
Kutokana na hilo, Rais Magufuli alisema kama wanafikiri kuwa na raia kwenye Jeshi la Polisi wanaliharibia jeshi, wahamishwe na wapelekwe utumishi.
Kutokana na hilo, Rais Magufuli alisema kama wanafikiri kuwa na raia kwenye Jeshi la Polisi wanaliharibia jeshi, wahamishwe na wapelekwe utumishi.
“IGP
kaorodheshe raia wote wanaofanya katika Jeshi la Polisi watoke.
Tuwapangie kazi nyingine kazi za kiraia. Ili kusudi hawa raia wanaokaa
kwenye nafasi za jeshi waondoke. Bila kufanya hivyo inawezekana
wataendelea kuwachafulia. Naomba hilo lishughulikiwe,” alisema.
Mbali
na agizo hilo, alimtaka IGP kufuatilia mtu aliyelipwa kati ya Sh20
bilioni hadi Sh60 bilioni kwa ajili ya kutengeneza sare za polisi tangu
mwaka jana, lakini hadi sasa bado hajakabidhi sare hizo.
“Tupate
hizo fedha zetu ili mkakomboe magari yenu. Ninategemea siku moja
waliohusika na hilo watapelekwa mbele ya haki,” alisema.
Mwigulu Nchemba
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba aliwataka walioapishwa kufanya kazi kwa bidii na uadilifu. “…Sheria isipofuata mkondo wake wananchi wanachukua sheria mkononi. Tuzuie hilo na kuhakikisha sheria zinafuatwa,” alisema.

Kamishna
wa maadili, Jaji mstaafu Salome Kaganda aliwashauri maofisa hao wa
Jeshi la Polisi kuunda kamati za maadili kwa ajili ya kusikiliza
manung’uniko yao.
IGP,
Mangu alimshukuru Rais kwa kupokea mapendekezo yao na kuahidi kuwa
atahakikisha maofisa hao wanatekeleza kiapo walichokula.