Tume
ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), itaanza kudahili wanafunzi waliomaliza
kidato cha sita wanaoomba kujiunga na vyuo vikuu kuanzia kesho.
Akizungumza
jana, Kaimu Mkurugenzi wa Udahili na Nyaraka wa TCU, Dk Kokubelwa
Mollel alisema udahili kwa wenye diploma utaanza Julai 31.
Dk
Mollel alisema kazi hiyo itaendelea kwa mwezi mzima ili kuruhusu
wananchi wengi zaidi kupata fursa ya kuomba kudahiliwa na udahili huo
utafanyika kwa njia ya mtandao.
Alisema
ili wanafunzi waweze kuelewa programu zinazotolewa na vyuo vikuu, tume
hiyo imeandaa maonyesho ya 11 yatakayofanyika kuanzia Julai 20 hadi 22,
mwaka huu.
Alisema
maonyesho hayo yatafanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es
Salaam na kufunguliwa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo
ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako.