Msanii
wa BongoFleva mwenye 'hit song' ya 'Mvumo wa Radi' Alikiba maarufu kama
King Kiba amefunguka na kudai yeye sio miongoni mwa wasanii
wanaotegemea kupata pesa kutoka katika 'views' za Youtube kama baadhi
yao wanavyofikilia vichwani mwao.
King
Kiba ametoa kauli hiyo ikiwa zimepita siku kadhaa tokea video yake mpya
ya 'Mvumo wa Radi' kushindwa kuendelea kuhesabu idadi ya watu
walioitazama jambo ambalo wengi wao walidai kuna mchezo anafanyiwa
msanii huyo ili asiweze kufikisha 'views' wengi kama ilivyokuwa kawaida
yake kila atowapo video.
"Hii ndio mara ya kwanza kunitokea tatizo hilo ila halijaweza kuniathiri kwa namna yeyote ile.
"Ila
nashukuru watu wamepata walichokuwa wanastahili nasio kwamba mimi
nategemea pesa kutoka 'Youtube views', mimi nafanya muziki najua wapi
napata pesa katika muziki wangu.
"Nilichokuwa nahitaji kiukweli ni mashabiki zangu waridhike na waelewe mimi ni msanii wa aina gani", amesema Alikiba.
Pamoja
na hayo, Alikiba ameendelea kwa kusema "tunajua kwamba kuna hizi
biashara za kuweka ma-robot katika 'Youtube' ili ionekane watu wana
'view' kwa wingi ila mimi binafsi ninaona ni utoto tu. Haitokuja kutokea
hata siku moja kwamba Alikiba ameweka 'robot' ili apate 'views' nyingi,
mimi nafanya muziki wangu kwa ajili ya watu na kwanini sasa nidanganye
watu".
Wimbo
wa Alikiba kwa sasa umetazamwa jumla ya watu milioni 1.2 na kushikilia
nafasi ya kwanza katika ya video zilizotazamwa kwa kiasi kikubwa kutoka
Youtube
0 comments:
Post a Comment