Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, amebainisha kuwa baba yake
ni moja kati askari kutoka Tanzania ambao wamepigana vita nyingi
kwaajili ya kutetea taifa ikiwemo vita ya kagera mwaka 1978.
Mh. Paul Makonda amesema hayo leo Mei 17, 2018 wakati wa alipokuwa
anatoa salamu kwa Rais Magufuli katika sherehe za ufunguzi wa kituo cha
uwekezaji cha SUMA JKT Mgulani Jijini Dar es salaam na kuongeza kuwa
alizaliwa na kulelewa katika kambi za jeshi
“Nikunong’oneze mheshimiwa Rais, mimi nimezaliwa kambini na baba yangu
ni miongoni mwa askari waliopigana vita nyingi ikiwemo vita ya Uganda na
mpaka ulemavu wake wa mguu ni kutokana na kazi ya kuipigania Tanzania”
amesema Makonda
Makonda aliongeza kuwa kutokana na kulelewa katika kambi za jeshi
imemsaidia kupata ujasiri wa kuongoza mkoa wa Dar es salaam wenye
changamoto nyingi na kuweza kufanya kuwa Jiji la raha Tanzania.
Katika tukio hilo, Rais Dkt Magufuli alizindua kituo cha uwekezaji cha
SUMA-JKT ambacho ndani yake kuna kiwanda cha Ushonaji, Maji, Chuo cha
Ufundi Stadi na Ukumbi wa Mikutano.
Thursday, May 17, 2018
TANGAZA HAPA KWA BEI NAFUU
0 comments:
Post a Comment