Na Loretha Laurence-WHUSM,Dodoma
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe
amempongeza mwanamitindo wa kimataifa Bibi. Flaviana Matata kwa juhudi
za kusaidia watoto wa kike kupata elimu kwa kuwawezesha vifaa muhimu
vya shule ikiwemo ada na madaftari.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana Jijini Dodoma Dkt. Mwakyembe amewataka
vijana wa kitanzania kuiga mfano wa mwanamitindo huyo ili kuchangia
katika ujenzi wa taifa.
“Nawasihi
vijana wengine wenye fursa kama za Flaviana Matata kuzitumia vizuri
kwa kuhakikisha jamii inanufaika na mafanikio waliyoyapata” ameongeza
Dkt. Mwakyembe
Aidha,
aliongeza kwa kueleza kuwa, Mwanamitindo huyo amekuwa ni balozi mzuri
katika kupeperusha bendera ya Taifa katika nchi mbalimbali za Ulaya.
Kwa
upande wake Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.
Juliana Shonza amempongeza Bibi. Flaviana kwa kuwa mfano bora kwa
watoto wa kike kwa jinsi ambavyo amekuwa akisaidia watoto wa kike
nchini.
Naye
Mwanamitindo wa Kimataifa Bibi. Flaviana Matata ameleza kuwa mbali na
kujishughulisha na mitindo, ameweza kuanzisha kampuni ya Flaviana Matata
Foundation ambayo inasaidia kutoa vifaa vya shule, ambapo hadi sasa
amefanikiwa kutoa vifaa zaidi ya 5000 katika shule mbalimbali nchini.
Anazidi
kueleza kuwa, Taasisi hiyo imefanikiwa kurabati shule mbalimbali kwa
kujenga madarasa na kusomesha wasichana 15 ambao wanamaliza kidato cha
sita mwaka huu na wengine watano bado wapo shule.
Hata
hivyo, Mwanamitindo huyo ameushukuru uongozi wa Wizara kwa jitihada za
wazi wanazozifanya katika kusimamia haki za wasanii na hivyo kurudisha
hadhi ya tasnia hiyo nchini.
0 comments:
Post a Comment