Wasanii
wa muziki wa dansi, Nguza Viking ‘Babu Seya’ na Johnson Nguza ‘Papii
Kocha’ wameshindwa kwenda nyumbani kwao Congo kwaajili ya shughuli za
kimila.
Wawili
hao baada ya kusamehewa kifungo chao mwishoni mwaka jana, waliahidi
kwenda nyumbani kwao kwa ajili kutembelea kaburi la mama yao mzazi.
Babu Seya amedai hawawezi kwenda nyumbani kwao kwa sasa kwa kuwa bado hawajapata pesa.
“Unajua
ukienda nyumbani unatakiwa kuwa na pesa, sisi bado tupo kwenye
mihangaiko ya pesa, mambo yakitulia tutaenda,” alisema Babu Seya.
Katika
hatua nyingine muimbaji huyo amewaomba wadau wa muziki kuidhamini show
yake ya kurudi rasmi kwenye muziki baada ya misukosuko ya muda mrefu ya
gerezani.
0 comments:
Post a Comment