Labels
Kiwanda
cha nyama cha Tanzania (TMC) kimepigwa faini ya Milion 5 baada ya
kukiuka kanuni za uhifadhi wa mazingira na kuchelewa kutekeleza agizo
walilopewa kuhakikisha wanafanyiakazi maagizo waliyopewa juu ya
kufanyiakazi kanuni za utunzaji wa mazingira ikiwemo kufanya tathmini
mazingira kabla ya kuanza kazi.
Akizungumza
wakati akikagua machinjio hayo na kiwanda hicho cha nyama Naibu waziri
wa nchi Ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira Kangi Lugola
Ameelezea kutoridhishwa na hali ya mazingira kiwandani hapo.
Akitoa
tamko hilo ,Naibu waziri Lugola alisema kuwa kulingana na sheria za
usimamizi na usafi wa mazingira ni sharti kiwanda hicho kitozwe faini
ili iwe fundisho kwa viwanda vingine kufuata taratibu ikiwa ni pamoja na
kufanya tathmini ya mazingira kabla ya kuanza shughuli za uzalishaji.
Pamoja
na mambo mengine Lugola alikiagiza kiwanda hicho kuelekeza taka ngumu
kwenye dampo la jiji lililopo Chidaya -Ntyuka ili kuepuka madampo yasiyo
rasmi yanayozagaa katikati ya jiji na kukuta mizoga ya nyama ikiwa
imezagaa maeneo mbali mbali.
Awali
akisoma taarifa kwa naibu waziri Lugola,Mtendaji Mkuu wa kiwanda hicho
Aron Luziga alizungumzia changamoto zilizopo kiwandani hapo kuwa ni
pamoja na mfumo wa maji taka usio rasmi kutokana na gharama kubwa ya
ujenzi pamoja na upatikanaji wa umeme wa uhakika hali inayokwamisha
shughuli za uzalishaji .
Alisema,hali
ya kukatika katika kwa umeme kiwandani hapo inakwamisha shughuli za
uzalishaji hivyo kuiomba serikali kuangalia namna ya kuboresha
miundombinu ya umeme ili kukidhi mahitaji .
"Lengo
la kiwanda hiki ni kuwa kinara katika uzalishaji wa nyama na
kusafirisha nchi nyingi zaidi duniani hii ikiwa ni pamoja na uchakataji
wenye kiwango kuendana na soko La kimataifa," alisema Luziga.
Wakati
huo huo Naibu waziri Kangi Lugola ameliagiza Baraza la usimamizi wa
mazingira la Taifa (NEMC) kushirikiana na uongozi wa jiji la Dodoma
kukagua kwa undani mifumo ya maji taka ya kiwanda cha kukamua mafuta ya
alizeti cha Sunshine kilichopo katika kijiji cha Zuzu.
Hatua
hiyo imekuja kutokana na kushindwa kuibaini mifumo ya majitaka
kiwandani hapo kutokana na kuwa kiwanda kimesitisha uzalishaji kutokana
uhaba wa malighafi kiwandani hapo.
Kutokana
na hayo Naibu waziri Lugola emeutaka uongozi wa kiwanda hicho kuingia
mkataba na wakulima ili waweze kupata malighafi ambazo zitawezesha
kiwanda hicho kuwa na uzalishaji wakati wote.
"Ni
kweli tunahitaji Tanzania ya viwanda,lakini viwanda hivyo vije kwa
kuzingatia sheria za mazingira ili kuyahifadhi na kwa manufaa ya vizazi
vijavyo," alisema.
Hata
hivyo alisema viwanda vinapaswa kuchochea wananchi kuondokana na
umaskini hivyo ni wajibu kushirikiana na wananchi bega kwa bega kupata
solo la uhakika.
0 comments:
Post a Comment