Serikali
kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
imewapa siku 45 watendaji wa soko la kimataifa la feri kuhakikisha
wanarekebisha miundombinu mibovu ambayo imekuwa kero kubwa kwa
wafanyabiashara wa maeneo hayo.
Hayo
yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo baada ya kufanya ziara ya
kushtukiza jana na kuona shimo kubwa katika eneo hilo ambalo kwa
tathmini ya mafundi wamesema inatakiwa shilingi milioni 36 ili
kulikarabati huku makusanyo ya ushuru ya soko hilo yakiwa zaidi ya
shilingi milioni 90 kwa mwezi hali iliyompelekea kuwaambia watendaji hao
wajitathimini kama wanatosha kuongoza
"Hapa
kuna uzembe uliopitiliza na ukiona uzembe kama huu katika vitu ambavyo
vya msingi vinavyohusu maisha ya watu, milioni 36 kwa shimo miaka miwili
na nusu halijazibwa huu ni uzembe na hii inaonesha hata katika
makusanyo yenu ya mapato kuna wizi mkubwa, huwezi kuniambia mmeshindwa
kuziba shimo kama hili kwa milioni 36", alisema Jafo.
Kwa upande wao wafanyabiashara wa soko hilo wamelalamikia huduma mbovu zilizopo katika soko hilo.
0 comments:
Post a Comment